Kutengeneza pesa kwa kutumia Facebook

Imekuwa ni kawaida kwa watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii kuitumia kuelezea mambo mengi sana. Wapo wanaozungumzia masuala ya kijamii, kiafya, kisiasa, kiuchumi, mahusiano, elimu za dini na kidunia, muziki na mambo mengi mbalimbali. Lakini leo nataka tuangalie jinsi unavyoweza kutumia mtandao wa facebook kutengeneza hela.

Kuna msemo wa Kiswahili unaosema kwamba “Biashara ni matangazo” msemo huu unakuwa dhahiri pale tunapoangalia barabarani mabango mbalimbali, matangazo kwenye television na hata kwenye mitandao ya kijamii. Watu wanatumia akili nyingi kutengeneza picha za kuvutia macho ya watazamaji au kutengeneza hata vikaragosi “Cartoon” vinavyotolea maelezo bidhaa zao. Je, vikisha tengenezwa hupelekwa wapi?
Baada ya kutengeneza picha zako za matangazo au vikaragosi, unaweza sasa ukasambaza kwenye mitandao ya kijamii na kuwafikia wateja moja kwa moja. Kwa kutumia facebook unaweka picha yako kwenye account yako au unaweza kutengeneza ukurasa ambao wenyewe utakuwa mahususi kwa kutangaza tu biashara unayoifanya. Lakini pia kuna makundi mengine mengi kwenye facebook ambayo yanafanya biashara kama ya kwako, hivyo unaweza kuingia kwenye kundi ambalo linazungumza masuala ya biashara na wewe ukaweka biashara yako.
Jinsi ya kutengeneza ukurasa wako wa facebook. Bofya hapa……kisha fuata maelekezo.
Baada ya kutengeza ukurasa wako wa facebook unaweza ukaupa uwezo wa kufikiwa na watu wengi kwa kasi na urahisi Zaidi kwa kufanya baadhi ya mambo ili kuupa uwezo.
Kitu cha kwanza ni kuupa uwezo “boosting page”, hii hufanyika kulingana na mahitaji yako binafsi. Unalipia kiasi cha pesa, kuanzia shilling 6,600/= za kitanzania na kuendelea. Hii inatokana na idadi ya watu ambao unahitaji kuwafikia.
Pia unaweza kutengeneza tangazo yaani “Facebook Ads” ambapo facebook wenyewe watakuwa wanakutangaza kulingana na watu amabao unachangia nao vitu unavyoviweka kwenye mtandao.


Kutengeneza pesa kwa kutumia Facebook Kutengeneza pesa kwa kutumia Facebook Reviewed by Unknown on 05:20:00 Rating: 5
Powered by Blogger.