Jinsi Ya Kuweka Bold Italic Na Tide Kwenye Whatsapp

Watu wengi husumbuka sana wanapoandika ujumbe kwenye app ya WhatsApp kutokana na hali kwamba herufi huwa na uzito sawa wa rangi katika hali ya kawaida. Mtindo huwa mmoja tuu, ila kuna namna ya kufanya kuwa tofauti.


Whatsapp: Bold, Italic na Strikethrough

Je, wajua unaweza kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo (Italic) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati (strikethrough) kwenye Whatsapp?

Unachohitaji kufanya kwanza kabisa ni kuwa na toleo la karibuni zaidi la app ya WhatsApp kwenye simu yako.

Kuweka Bold


Ili kukoza rangi kwenye herufi (kufanya bold), unahitajika kutanguliza neno lako na alama ya nyota na kisha kuhitimisha na alama ya hiyo hiyo ya nyota kwa mfano ukiandika *bold* itatokea ikiwa bold.
Whatsapp: Ujumbe ambao ni bolded

Whatsapp: Jinsi ya kufanya ili ujumbe wako uwe bolded  

Kuweka Italic

Ili kufanya herufi zako kuwa za mlazo (italic), unahitajika kutanguliza na mstari sakafu (underscore) na kuhitimisha na alama iyo hiyo. Kwa mfano ukiandika “_italics_” itatokea ikiwa Italics.
Jinsi ya kufanya ili ujumbe wako uwe katika mfumo wa Italics
Jinsi ya kufanya ili ujumbe wako uwe katika mfumo wa Italics

Kuweka strikethrough(tide)

Ukitaka kuweka alama ya kukata kati kwenye herufi zako, unahitajika kuanza na alama ya mawimbi  [tilde (~)] na kuhitimisha na alama iyo hiyo. Kwa mfano ukiandika “~strikethrough~” itatokea ikiwa na mstari uliokata herufi kati.
Ujumbe ukiwa katika mfumo wa strikethrough
Ujumbe ukiwa katika mfumo wa strikethrough

Kuunganisha mitindo

Unaweza ukataka kuunganisha mitindo, mfano utake  maandishi yako kuwa na bold, strikethrough na Italic kwa wakati mmoja utahitajika kutumia alama za unachohitaji katika kuanza neno lako na kuhitimisha.
Mfano, ukiandika “~_*bolditalics*_~” inafaa kutokea ikiwa bold-italics pamoja na strikethrough.
Mfano ujumbe wenye bold, italic na strikethrough
Mfano ujumbe wenye bold, italic na strikethrough

Je, umefanikiwa kuweza kufanya maandishi yawe bold, italic, strikethrough au vyote kwa pamoja?

Niandikie comment yako kama umefanikiwa au wapi hujanielewa na mimi nitakujibu. CloudClan daima tunajali wasomaji wetu

Jinsi Ya Kuweka Bold Italic Na Tide Kwenye Whatsapp Jinsi Ya Kuweka Bold Italic Na Tide Kwenye Whatsapp Reviewed by Unknown on 02:17:00 Rating: 5
Powered by Blogger.